Messi aanza kwa mkosi Barca

Muktasari:

  • Lionel Messi alifunga bao la penalti lakini Marc-Andre ter Stegen akafunga la pili na Giovani lo Celso akaifungia Betis bao la tatu, Arturo Vidal akaifungia Barca lakini Sergio Canales alifunga la nne, kabla ya Messi kufunga bao la tatu.

Barcelona, Hispania.NI kama vile kiungo mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi ameanza kwa mkosi baada ya kuwa nje ya dimba kwa muda tangu alipoteguka mkono.

Juzi Jumapili alicheza kwa mara ya kwanza, lakini timu yake ilichezea kichapo cha mabao 4-3 dhidi ya Real Betis kwenye uwanja wake wa Nou Camp.

Junior Firpo aliifungia Betis bao la kuongoza dakika ya 20 kabla ya veterani, Joaquin kufunga bao la pili.

Lionel Messi alifunga bao la penalti lakini Marc-Andre ter Stegen akafunga la pili na Giovani lo Celso akaifungia Betis bao la tatu, Arturo Vidal akaifungia Barca lakini Sergio Canales alifunga la nne, kabla ya Messi kufunga bao la tatu.

Vijana wa Ernesto Valverde bado wako kileleni kwenye msimamo wa La Liga, wakiwa na pointi moja mbele ya Sevilla, Atletico Madrid na Alaves.

Hata hivyo, katika mchezo huo, Ivan Rakitic alitolewa kwa kadi ya pili ya njano washindi wakiwa mbele kwa mabao 3-2.

Barca mara ya mwisho kupoteza ilikuwa Septemba 10, 2016, ilipochapwa 2-1 nyumbani dhidi ya Alaves.

Betis imepoteza mara zote ilipocheza na Barcelona Nou Camp na haikuwahi kushinda kwenye uwanja huo kwa zaidi ya miaka 20.

Huko Real Madrid imepunguza wigo wa pointi katika msimamo wa La Liga na kuwa pointi nne na Barcelona baada ya kuinyuka Celta Vigo mabao 4-2.