Merson aiondoa Man United Top 4

Muktasari:

  • Miamba hiyo ya Old Trafford iko nafasi ya sita nyuma ya Arsenal yenye pointi 66 kabla ya mchezo wa jana Jumapili huku Tottenham ikiwa na pointi 67 na iko nafasi ya nne.

LONDON,England.MANCHESTER City ilipaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England kwa kuilaza Tottenham Hotspurs bao 1-0 juzi Jumamosi na kuiacha Liverpool kwa pointi moja (kabla ya mchezo wa jana), lakini mkongwe wa soka, Paul Merson kaibuka kivyake na kusema hata iweje, Manchester United itakuwa ya sita hadi mwisho wa msimu.

Asilimia kubwa ya timu zimeshacheza mechi 34 na kila mmoja ana mechi nne zilizosalia kukamilisha ratiba.

Arsenal pekee ilikuwa na mechi 33 na jana ilikuwa ikicheza na Crystal Palace.

Merson alisema Man United ambayo jana ilipigwa 4-0 na Everton iko mbali sana kwenye msimamo na hata Top Four wataisikia kwenye bomba.

Miamba hiyo ya Old Trafford iko nafasi ya sita nyuma ya Arsenal yenye pointi 66 kabla ya mchezo wa jana Jumapili huku Tottenham ikiwa na pointi 67 na iko nafasi ya nne.

Alisema Manchester United kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la FA ni kwamba kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer kinapitia wakati mgumu kwa sasa.

Pamoja na kuwa msimu wa 2018-19 bado kuhitimika, inaweza kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya kutokana na pointi zake, lakini Merson amefuta hilo na kusema mwaka huu Man United hawana chao kutokana na upepo ulivyo.