McGregor: Kipigo nilichopewa kilikuwa halali kabisa

Tuesday October 23 2018

 

Bondia Canor McGregor ametoa kali ya mwaka baada ya kuibuka na kueleza kwamba kipigo alichopokea kutoka kwa mwenzake, Khabib Nurmagomedov kilikuwa halali.

Bondia huyo alisema licha ya kipigo hicho kikali alichokipata lakini ameapa kurudia makosa ambayo aliyafanya.

Alisema bondia huyo mpinzani wake ni kwamba alimuotea na kumpatia kichapo katika eneo ambalo baada ya kupata nafasi alitumia vyema.

Bondia huyo alisema hawezi kumdharau Khabib lakini asitarajie kuwa anaweza kumvuruga kwa mara nyingine ikitokea wakakutana.

McGregor alijikuta akipokea kichapo kutoka kwa Mrusi huyo katika raundi ya nne pambano la uzito wa juu lililofanyika Oktoba 6.

Hata hivyo baada ya kupoteza mchezo wake, alituma kwenye ukurasa wake wa Istagram akionyesha jinsi ambavyo alipokea kichapo.

Advertisement