Mbosso afunguka majanga yake

Muktasari:

Matukio makubwa yalikuwa yakiwaumiza wengi kutokana na umaarufu waliokuwa nao hao wanaopatwa na matatizo ambayo ni misiba mikubwa.

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, kutoka katika rebo ya (WCB), Mbwana Yusuph 'Mbosso' amesema mwaka 2018 aliandamwa na jinamizi la vifo kitu ambacho kilikuwa kinampa changamoto.
Akizungumza na Mwanaspoti, alisema jinamizi hilo lilizama katika siku zake muhimu za matukio makubwa kwenye sanaa yake ya muziki ambapo alipatwa na mikosi kila anapotoa video za kazi zake mpya.
Alisema kila akipanga kutoa video yake kulikuwa kunatokea na matukio makubwa sana na yalikuwa yakiwaumiza wengi kutokana na umaarufu waliokuwa nao hao wanaopatwa na matatizo ambayo ni misiba mikubwa.
"Mwaka 2018 nilitiwa unyonge kutokana na kutokea na misiba mikubwa kila ninapofanya matukio yangu makubwa ya kimuziki naamini hakuna anayelifanamu hili ila kila nikitoa wimbo, lazima utokee msiba. Kila nikitoa wimbo, kila nikiweka video," alisema.
"Nakumbuka kipindi natoa Nadekezwa kulitokea Msiba wa mtoto wa dada mmoja anaitwa Muna. Kipindi nakuja kutoa Nipepee kulitokea msiba wa mzee Majuto. Nilivyotoa Hodari kulitokea ajali ya MV Nyerere, nikawa nawaza kwanini zinatokea changamoto kama hizi? ilinipa mawazo sana,"
Alisema kutokana na changamoto hiyo alikuwa anashindwa kuzifanyia matangazo nyimbo hizo ili watu waweze kufahamu kunakitu kipya amekifanya lakini anamshukuru mungu ziliweza kufanya vizuri katika mitandao ya kijamii hasa Youtube ilitazamwa sana.