Mbongo huyu mawazo yake kutua Everton tu

Muktasari:

  • Michuano hiyo itakayofanyika jijini Dar es Salaam itahusisha vigogo vinane vya soka kutoka Tanzania na Kenya na itatimua vumbi kuanzia Januari 22 hadi 27.

KIUNGO wa Bandari ya Kenya, Hamis Abdallah ameanza kuwa na mawazo ya kucheza na Everton ya England baada ya kutua na timu yake kwenye Kombe la SportPesa litakalofanyika kwa mara nyingine tena hapa Tanzania.

Hamisi alisema lengo lao ni kutwaa ubingwa wa kombe hilo ili wakajifunze kwa vitendo kwa wenzao waliowatangulia kwenye soka, Everton.

“Hii ni nafasi muhimu kwetu kwa hiyo sio vizuri kama tutaipoteza tumetoka Kenya ambako tumeuanza msimu vizuri ni wazi damu zetu bado zimechangamka na tuko tayari kwa ushindani.

“Kwa kweli hakuna timu ambayo tunaihofia na ukizingatia hii ni mara yetu ya kwanza kupata nafasi ya kushriki michuani hiyo, lazima watu watambue kuwa hutujaja huku kutembea,” alisema Hamis

Michuano hiyo itakayofanyika jijini Dar es Salaam itahusisha vigogo vinane vya soka kutoka Tanzania na Kenya na itatimua vumbi kuanzia Januari 22 hadi 27.

Kombe la Sportpesa linashirikisha watani wa jadi Simba na Yanga, Mbao FC pamoja na Singida United kutoka Tanzania na vigogo wa soka la Kenya Gor Mahia, AFC Leopard, Bandari FC na ving’ang’anizi Kariobangi Sharks.