Mbelgiji asuka mchongo mpya Simba

Muktasari:

Simba wanaendelea na maandalizi ya mechi ya kirafiki ambayo itachezwa kesho Ijumaa dhidi ya Big Bullets mabingwa mara 12 wa Ligi Kuu ya Malawi ambao utapigwa katika uwanja wa Taifa.

Kocha wa Simba Mbelgiji Patrick Aussems amesema kwamba maandalizi ambayo wanayafanya wakati huu si kwa ajili ya mashindano ya kimataifa.
Aussems anasema nusu ya wachezaji wake wa kikosi cha kwanza hawapo katika timu wapo katika majukumu ya timu zao za Taifa na hapo watakaporudi kazi itaanza upya kabisa.
"Sipo na kikosi kamili nikisema kwamba haya mazoezi ambayo tunayafanya sasa ni kwa ajili ya Kimataifa itakuwa si kweli ila watakapokuwa wote maandalizi ya michuano hiyo yataanza tena ya hali ya juu," alisema.
"Hata mechi ambazo tunacheza sasa ni kwa ajili ya kuwapa nafasi wachezaji ambao hawajatumika na wanauwezo wa kuona walichokuwa nacho ili kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.
"Mechi hii ambayo tunacheza ni ya kirafiki lakini ni ya kimataifa kwahiyo tutaanza kujijengea mazoea ya kucheza mechi hizo kabla na yanafanyika yote haya ili wachezaji wote watumike," alisema Aussems.