Mbaraka Yusuph mzigoni leo

Muktasari:

  • Kocha wa Namungo FC, Novatus Fulgence alisema amefurahishwa na uongozi wa Azam kumpatia mchezaji huyo ambaye anawapa nguvu ya mapambano ya FDL.

NYOTA mpya wa Namungo FC, Mbaraka Yusuph anatarajia kuanza mazoezi leo Jumatatu na kikosi chake kipya kujiandaa na Ligi Daraja la Kwanza (FDL).

Chipukizi huyo ametua kwenye kikosi hicho akitokea Azam FC kwa mkopo ili kunoa makali yake baada ya kukosa namba kwenye mipango ya Kocha, Hans Van Pluijm wa Azam.

Kocha wa Namungo FC, Novatus Fulgence alisema amefurahishwa na uongozi wa Azam kumpatia mchezaji huyo ambaye anawapa nguvu ya mapambano ya FDL.

“Ujio wa mchezaji huyu utaongeza nguvu zaidi kwa sababu ni mmoja kati ya wachezaji niliokuwa nawaheshimu, hivyo atakuwa chachu ya mafanikio ya Namungo,”

“Wachezaji wote walikuwa mapumziko mafupi na leo Jumatatu ndio tunaanza programu kamili na baada ya siku kadhaa tutaona jinsi ya kukiweka fiti zaidi kikosi kwa kucheza michezo ya kirafiki,” alisema Fulgence.

Aliongeza atahakikisha anasaka wachezaji wengine wanne wa kuongeza nguvu, nafasi ya mabeki atasajili wawili, kiungo na mshambuliaji atachukua mmoja mmoja kila nafasi nili kupata uwiano mzuri.