Mbao FC yaichimba mkwara Gor Mahia

Muktasari:

Timu hizo zitavaana kesho Jumatano kwenye mchezo wa mapema mchana kabla ya kuipisha Simba kumalizana na AFC Leopards baadaye jioni.

MWANZA. MBAO imetoka kupoteza mchezo wa Ligi Kuu mbele ya JKT Tanzania, lakini kocha wake ameichimba mkwara mapema Gor Mahia ya Kenya akidai isitarajie kuondoka na taji la SportPesa kwa mara nyingine katika ardhi ya Tanzania.

Timu hizo zitavaana kesho Jumatano kwenye mchezo wa mapema mchana kabla ya kuipisha Simba kumalizana na AFC Leopards baadaye jioni.

Kocha wa Mbao, Ali Bushiri ‘Benitez’ alisema akili zao zipo kwenye michuano hiyo wanayoshiriki kwa mara ya kwanza wakiwa na kiu ya kuandika rekodi ya kushiriki kwa mara ya kwanza na watetezi hao wasitarajie mteremko kutoka kwao.

“Ni mchezo muhimu kwetu, tutapambana kadiri ya uwezo wetu ili kuifunga Gor Mahia na tusonge mbele, tumepata bahati ya kushiriki michuano hii, hivyo tunapaswa kuonyesha kitu tofauti,” alisema Benitez.

Kocha huyo aliongeza watamkosa Evaligestus Mujwahuki aliyeumia wakati wa mechi yao na Singida United.