Mbao FC yatambulisha uzi mpya

Friday August 10 2018

 

By THOMAS NG'ITU

Dar es Salaam. KLABU ya Mbao FC imetambulisha jezi zao za watakazotumia nyumbani na ugenini msimu huu.

Msemaji wa kampuni ya GF Truck Equipment, Kulwa Bundala, alisema jezi hizo wamezitoa ikiwa ni sehemu ya mkataba wao wa awali waliosaini na timu hiyo.

"Jezi hizi ni sehemu ya mkataba wetu na Mbao kwa hiyo tupo katika sehemu ya kutimiza majukumu yetu kwa kutoa vifaa," alisema Bundala.

Mwenyekiti wa Mbao, Solly Njashi alisema anashukuru hatua iliyochukuliwa na wadhamini wao kuelekea kuanza kwa Ligi Kuu.

"Wadhamini wetu tupo nao bega kwa bega na tunawashukuru katika hili kwasababu walianza kiwa nasi tangu katika mambo yanayohusu klabu nzima," alisema Njashi.

Advertisement