Mavunde awapiga kijembe Simba

Saturday June 15 2019

 

By Thomas Ng'itu

MWENYEKITI wa kamati ya kuchangisha pesa klabu ya Yanga, Anthony Mavunde amewapiga kijembe watani wao wa jadi Simba kushindwa kumtambulisha mchezaji wao majira ya saa 7 mchana kama walivyoahidi.
Awali msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara aliweka picha katika mtandao wake wa Instagram akisema saa 7 mchana leo Ijumaa wataisimaisha nchi na wafuasi wake wawe makini  muda huo kuangaliwa ukurasa wa Simba wa Instagram.
Mavunde alisema hayo wakati akiwa anatoa shukrani kwa mashabiki na wanachama ambao walikuwa wanaichangia timu hiyo muda wote.
"Jamani hivi sasa ni saa 9 mbona bado nchi haijasimama mpaka hivi sasa, kulikoni hukoo," alihoji na ndipo shangwe ziliiubuka ukumbini hapa.
Hata hivyo, inadaiwa Simba wamepigwa bao na Yanga kwani mchezaji Juma Balinya ambaye alikuwa asajiliwe na Wekundu wa Msimbazi tayari amesaini Yanga mkataba wa miaka miwili.
Pia mchezaji huyo alikuwepo muda wote ukumbini hapa pamoja na mwenzake Abdulaziz Makame.

Advertisement