Mauritania yatangaza kikosi cha maangamizi AFCON

Muktasari:

  • Timu hiyo inashiriki kwa mara ya kwanza kucheza fainali za Mataifa ya Afrika tangu kupata uhuru wake

Nouakchott, Mauritania. Mauritania imetangaza kikosi cha wachezaji 23, kitakachoshiriki fainali za Mataifa ya Afrika nchini Misri kuanzia Juni 21 hadi Julai 21.

Mauritania imepangwa kundi gumu pamoja na Tunisia, Mali na Angola. Waanza kwa kucheza mechi ya kwanza Juni 24 dhidi ya Mali kwenye Uwanja wa Suez.

Kikosi hicho kumemjumuisha beki wa AJ Auxerre, Abdul Ba pamoja na nyota wa Valladolid, El Hacen El Id.

Pia kikosi cha wachezaji wa akiba chenye wachezaji saba kimetangaza.

Kikosi:

Makipa: Suleiman Brahim (FC Nouadhibou), Namori Diaw (ASC Kedia), Babacar Diop (AS Police)

Mabeki: Abdoul Ba (AJ Auxerre, Ufaransa), Bakary Ndiaye (Difaâ Hassani of El Jadida, Morocco), Sally Sarr (Servette FC, Uswisi), Diadié Diarra (CS Sedan Ardennes, France), Harouna Sy (Grenoble Foot 38, Ufaransa), El Mostapha Diaw (Nouakchott Kings), Aly Abeid (Agrupación Deportiva Alcorcón, Hispania), Abdoul Kader Thiam (US Orleans, Ufaransa)

Viungo: Mohamed Dellah Yaly (DRB Tadjenanet, Algeria), Ibréhima Coulibaly (Grenoble Foot 38, Ufaransa), Dialo Guidileye (Elazığspor Kulübü, Uturuki), Khassa Camara (Xanthi FC, Ugiriki), Alassane Diop (Hajer FC, Saudi Arabia), Abdoulaye Gaye (Nouadhibou FC), El Hacen EL Id (Real Valladolid, Hispania)

Washambuliaji: Adama Ba (Giresunspor Kulübü, Uturuki), Ismail Diakhite (US Tataouine, Tunisia), Moulaye Ahmed Khalil “Bessam” (AS Gabès, Tunisia), Souleymane Anne (FC Aurillac Arpajon CA, Ufaransa), Hemeya Tanjy (FC Nouadhibou)

Kikosi cha akiba:

Kipa: Assane Aly (Red Star FC, Ufaransa)

Mabeki: Hamza Jawar (USON Mondeville, Ufaransa), Ousmane Samba (JA Drancy, Ufaransa)

Viungo: Abdallahi Mahmoud (Deportivo Alaves, Hispania), Idrissa Thiam (ASAC Concorde)

Washambuliaji: Amadou Niass (Salam Zgharta, Lebanon), Mohamed Abdallahi Soudani (DRB Tedjenanet, Algeria)