Mastraika Simba bado

Tuesday February 12 2019

 

By Thobias Sebastian

Dar es Salaam. Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika katika mechi ya Ligi ya mabingwa Afrika kati ya Simba na Al Ahly kilimalizika bila kufungana.

 Simba ambao katika mechi ya kwanza dhidi ya wapinzani wao nchini Misri walikubali kufungwa mabao 5-0 lakini katika mechi hii Simba wakiwa nyumbani walionekana kuimarika tofauti na mechi iliyopita ambapo kipindi cha kwanza tu walikuwa wameshakula tano.

 Simba walishindwa kupata bao licha ya kupata nafasi tatu ambazo kama wangeongeza umakini walikuwa na uwezo wa kufunga.

Nafasi ya kwanza ilikuwa dakika 9, Emmanuel Okwi aliwapiga chenga mbeki wa Al Ahly na kupiga shuti ambalo lilinyakwa na kipa.

Maddie Kagere alipata pasi nzuri mbili dakika ya 12, ambapo alishindana na walinzi wa Al Ahly ambapo alipata nafasi na kupiga shuti  lililopanguliwa na kipa na kuwa kona.

  Kagere alifanya hivyo tena dakika 40, baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Chama na kupiga shuti ambalo lilipanguliwa na kipa na kuwa kona tena.

Simba walifanya mabadiliko dakika 39, kwa kumtoa Asante Kwasi na kuingia nahodha msaidizi Mohamned Hessein 'Tshabalala'. Al Ahly wao walifanya mashambulizi ya kushtukiza lakini muda mwingi walikuwa chini ya ulinzi wa Simba.

Kama Simba wangeweza kuongeza umakini katika nafasib walizopata haswa mastraika wait wawili Okwi na Kagere wangeweza kumaliza kipindi cha kwanza wakiwa mbele.

Advertisement