Mastaa hawa pasua kichwa Simba

Monday September 10 2018

 

By OLIPA ASSA

Dar es Salaam. Kocha wa Simba, Patrick Aussem ameweka wazi nyota anawaona ni roho ya timu ni Pascal Wawa, Emmanuel Okwi, John Bocco, Meddie Kagere, Aishi Manula, Shiza Kichuya, Erasto Nyoni.

Zipo mechi ngumu wakikosekana hao naona kabisa kunakuwa na pengo kubwa, kutokana na uzoefu wao wa kupambana kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri.

Aussem anadadavua kuwa upana wa kikosi chake unafanya wachezaji ambao hawakuanza kupata nafasi ndani ya kikosi cha kwanza, awajaribu kwenye mechi za kirafiki na za ligi ambazo anakuwa hana cha kupoteza.

"Wapo wachezaji ambao nawategemea kwenye mechi ngumu kuhakikisha kwa hali na mali wanatoka na matokeo ambayo yana manufaa na timu, lakini nikiona tayari nina matokeo na hatuna cha kupoteza pia nawapa nafasi wale ambao hawakuanza kwenye kikosi cha kwanza.

"Naamini katika safari ya msimu huu tunaweza tukafanya vitu vikubwa na vya tofauti kwa sharti la kutumia vizuri kikosi nilicho nacho," alisema Mbelgiji huyo.

 

 

Advertisement