Mastaa Ulaya wamfariji Welback

Muktasari:

Kiungo huyo ambaye kwa sasa anaichezea Villarreal ya Hispania amemtakia apone haraka kupitia  mtandao wake wa kijamii wa Istagram baada ya mshambuliaji huyo kuumia kwenye mchezo uliomalizika kwa suluhu.

BAADA ya Danny Welbeck wa Arsenal  kumia vibaya jana kwenye mchezo wa Europa Ligi  dhidi ya  Sporting Lisbon, kiungo wa zamani wa timu hiyo, Santi Cazorla ametopa pole kwa mshambuliaji huyo.

Kiungo huyo ambaye kwa sasa anaichezea Villarreal ya Hispania amemtakia apone haraka kupitia  mtandao wake wa kijamii wa Istagram baada ya mshambuliaji huyo kuumia kwenye mchezo uliomalizika kwa suluhu.

Maneno hayo yalikuwa yakisomeka: “Pona haraka rafiki yangu. Kuna vitu vingi vya thamani kwenye soka lakini natambua kuwa kuwa wewe ni shupavu na utapona haraka,kila la kheri mtu wangu.”

Welbeck  alipata majeraha  hayo dakika ya 30  ya mchezo huo baada ya kashikashi za kuucheza mpira kwa kichwa.

Summary

Welbeck amekuwa na historia ya kupata majeraha ya mara kwa mara, mshambuliaji huyo   anakumbukwa kwa kuikosa kwake michuano ya mataifa ya Ulaya, 2016 kutokana na majeraha aliyoyapata akiwa na Arsenal.