Masoud afunguka mazito Msimbazi

Muktasari:

  • Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems ana mpango wa kuwatenganisha washambuliaji watatu wa kikosi chake, John Bocco, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi katika uchezaji kwa sababu tangu aanze kufanya hivyo hajapata matokeo mazuri.

KABLA ya keshokutwa Jumatano, Kocha Masoud Djuma atakuwa ameshaondoka nchini kama alivyopanga, labda tu itokee mengine, lakini Mrundi huyo ameamua kuvunja ukinywa juu ya kutimuliwa kwake Msimbazi, akiwatuliza Wana Msimbazi.

Kocha Masoud amesitishiwa mkataba wake wa miaka miwili, akiwa ameutumika muda wa mwaka mmoja na tayari ameshamalizana na mabosi wake, baada ya tangu mapema kutambua hatma yake ndani ya klabu hiyo ilikuwa ndogo, ila alikuwa akiendelea na kazi kwa vile alikuwa ndani ya mkataba huo aliosaini Oktoba mwaka jana.

Mabosi wa Simba wamethibitisha kuachana na Masoud na wameweka wazi kuwa watamlipa stahiki zake zote kutokana na makubaliano ya mkataba wake na wao, lakini tangu juzi Ijumaa mkataba ulivyositishwa, kocha huyo alikuwa mgumu kuzungumza.

Hata hivyo jana Jumapili Masoud aliliambia Mwanaspoti kuwa, alikuwa anaipenda Simba na ataendelea kuipenda na kilichompata ni changamoto za kazi zipo kila sehemu hivyo hana budi kukubaliana na hali halisi iliyotokea kwake.

“Haya yametokea ni mambo ya kawaida kwenye kazi na ipo sehemu yoyote. Ninachotaka kuwaambia Wanasimba nawashukuru kwa ushirikiano wao mkubwa na wajue nawapenda sana, sina chuki wala hasira nao.” alisema Masoud.

“Waelewe kwamba kila jambo hupangwa na Mwenyezi Mungu ambaye pia ndiye atakayedhihirisha ukweli wa jambo hili, nikizungumza mimi ni wazi nitaonekana najitetea, acha tuliache jinsi lilivyo. Kama nilivyokuja walinipokea basi nitawaaga siku ya kuondoka kwani kwa sasa bado nipo Tanzania,” alisema Djuma wakati akielekea kuswali Swala ya Insha karibu na eneo analokaa la Kunduchi, jijini Dar es Salaam.

Dalili za kutimuliwa kwa Kocha Masoud aliyeletwa na Simba ili kuchukua nafasi ya Jackson Mayanja, zilianza baada ya kudaiwa hakuwa anaiva na Kocha Mkuu, Patrick Aussems aliyeamua kumuacha katika mechi ya kwanza ya ugenini mjini Mtwara.

Masoud alibaki Dar es Salaam na wachezaji ambao pia hawakuwa kwenye mipango ya Aussems ikiwemo safari ya Kanda ya Ziwa kucheza dhidi ya Mbao na Mwadui.

Pia aliendelea kubaki jijini Dar es Salaam ikidaiwa anawafuatilia Yanga ambao walicheza nao wikiendi iliyopita na kutoka suluhu na ndiyo ilikuwa mechi yake ya mwisho.

MO KUNG’OA KIGOGO

Katika hatua nyingine, kama ulikuwa unadhani baada ya kuondoka kwa Kocha Masoud kazi imeisha Msimbazi, umekosea, kwani Bilionea wa Simba, Mohammed ‘MO’ Dewji ameendelea kulipangua benchi la ufundi la timu hiyo wakijiandaa kumng’oa kigogo mwingine.

Habari za kuaminika ndani ya Simba zinasema baada ya kuondolewa kwa Masoud kwa sasa ni zamu ya mwingine kung’olewa Msimbazi, baada ya kuelezwa wamemfuata Daktari kutoka India ili kusaidia masuala ya kitababu kwa nyota wa klabu hiyo.

Imeelezwa kuletwa kwa daktari huyo bingwa wa sekta ya michezo kutoka India ni mipango ya kuboresha benchi kama alivyowahi kunukuliwa MO Dewji kwenye mkutano wake wa kumtangaza kuwa Mwekezaji wa klabu hiyo katika mfumo wa hisa.

Inaelezwa ingawa kwa sasa hakuna mpango ya kutafutwa kwa kocha wa kuziba nafasi ya Masoud lakini mipango ni kuwatoa baadhi ya watu wa benchi la ufundi ili liwe bora na la kisasa zaidi.

Kwa sasa Daktari wa Simba ni Yasin Gembe ambaye inaelezwa atakapotua mtaalam kutoka India atasaidiana naye, huku taarifa nyingine zikidokeza kuwa huenda ikawa safari kwa daktari huyo.

Habari kutoka ndani ya Simba zinasema Makocha wa Simba wenye uhakika kikosini ni Mbelgiji, Aussems na KOcha wa Viungo, Zren Adel raia wa Uturuki, japo pia yupo Kocha wa Makipa, Muharami Mohammed “Shilton’.

“Gembe huenda akabadilishiwa majukumu mengi ama akabaki kumsaidia huyo jamaa anayeletwa. Haya ni mabadiliko tu ya kuboresha benchi.