VIDEO: Mashabiki wasubiri mechi Stars kwa saa 9

Muktasari:

Stars itacheza mechi yake ya mwisho ya makundi ya Kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) Leo saa 12 jioni ambapo kama itashinda itajiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu ikisikilizia matokeo ya Cape Verde na Lesotho.

Dar es Salaam.UNAACHAJE kuipenda Stars kwenye mchezo kama huu! ndiyo kauli ya mashabiki wa soka nchini ambao wanaendelea kumiminika kwenye uwanja wa Taifa kwa ajili ya kuisapoti Taifa Stars.
Stars itacheza mechi yake ya mwisho ya makundi ya Kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) Leo saa 12 jioni ambapo kama itashinda itajiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu ikisikilizia matokeo ya Cape Verde na Lesotho.
MCL Digital iliyofika uwanja wa Taifa mapema iliwashuhudia mashabiki wakimiminika uwanjani kushuhdia mchezo huo ambao mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Baadhi ya mashabiki walisema wamefika kwenye uwanja wa Taifa saa 3 Asubuhi wakisubiri mchezo wa saa 12 jioni.
"Nilikuwa natamani siku ifike, hivyo jana sijalala, nilipoamka cha kwanza ilikuwa nmi safari ya uwanjani," alisema Mtanzania, Kassim Haidary.
Mtanzania mwingine, Jackosn Patrick alisema amefika uwanjani Asubuhi, sababu hakutaka kusimuliwa chochote kuhusu mchezo huo.
"Milango ilipofunguliwa tu nilikuwa uwanjani, sioni tabu kukaa hata masaa 12 kusubiri mchezo kama huu wa timu yangu ya taifa," alisema.
Hadi saa nane mchana baadhi ya majukwaa ya mzunguko wa Orange upande wanaokaa mashabiki wa Yanga yalikuwa yamejaa.