Mashabiki wa michezo kuendelea kufurahia EPL

Muktasari:

Ofa imeanza mwezi huu itaendelea kwa muda wa miezi miwili hadi  mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu.

Dar es Salaam. Punde tu baada ya kumaliza ofa mahsusi ya kufunga mwaka iliyokuwa ikifahamika kama ‘’Muda wa   kukiwasha na DStv’’ MultiChoice Tanzania leo imetangaza neema kwa wateja wake wapya watakaojiunga na DStv katika msimu huu wa wapendanao ambapo watajipatia zawadi kabambe ya kifurushi cha DStv Family kwa kipindi cha miezi miwili !

  Alisema kampuni yao itaendelea kuonyesha  ligi  maarufu kama Serie A, La Liga, Ligi kuu ya Uingereza.

Ofa hiyo maalumu ijulikanayo kama ‘Jiunge na Family ya DStv’ ambayo imeanza mwezi huu itaendelea kwa muda wa miezi miwili hadi  mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu. Katika kipindi hicho wateja wote wapya wa DStv, wataweza kupata vifaa vyote vya DStv kwa shilingi  79,000 tu na kisha kupata ofa ya kifurushi cha DStv Family cha miezi miwili.

Akizungumza wakati wa uzinduzi  wa ofa hiyo katika ofisi za MultiChoice Tanzania, Meneja Masoko Alpha Mria amesema kuwa ofa hii ni muendelezo wa ofa kedekede zinazoletwa na kampuni ya MultiChoice kwa wateja wake mara kwa mara.

Amesema tofauti na ofa iliyopita ya muda wa kukiwasha na DStv ambapo mteja alikuwa anapatiwa mwezi mmoja wa kifurushi cha DStv Bomba 19,000/-  sasa hivi ofa ya kifurushi imeongezwa thamani hivyo mteja mpya sasa anapata ofa ya kifurushi cha DStv Family 39,000/-  tena siyo kwa mwezi mmoja tu, bali miezi miwili.

‘’Tunatambua  kuwa huu ni mwanzo wa mwaka na majukumu huwa ni mengi hivyo tumeamua kuwatunuku wateja wetu wanaojiunga nasi wakati huu kwa kuwazawadia kifurushi cha Family chenye chaneli zaidi ya 90 kwa miezi miwili” alisema Alpha.

“Kwa kifurushi hiki, mteja wetu atafurahia  maudhui mbalimbali ikiwemo tamthlia maarufu za ndani na nje, michuano ya ligi maarufu za soka duniani kama ligi ya Uingereza, Ligi ya Hispania (La Liga) Ligi ya Italia (Serie A), michezo na burudani nyingine kadha wa kadha kama mieleka, Taikondo, Ndondi, muziki bila kusahau Habari na vipindi vya elimu,” alisema.

Aliongeza kuwa kampuni yao itaendelea kuonyesha  ligi  maarufu kama Serie A, La Liga, Ligi kuu ya Uingereza, burudani ya mieleka WWE na  tamthilia kali za kitanzania kama HUBA, Kapuni, Rebeca, Kitimtim na kipindi maarufu cha umbea maarufu kama Shilawadu Xtra na vingine vingi ndani ya Maisha Magic Bongo DStv channeli (160).

Kwa upande wake, Mkuu wa Mauzo na Usambazaji Salum Salum amesema ofa hiyo ni kwa wateja wote wapya wanaojiunga na DStv kuanzia leo na kwamba ofa hiyo ni kwa nchi nzima. “Ofa hii ni kwa nchi nzima. Popote mteja alipo anaweza kupata huduma zetu kwani tuna mawakala nchi nzima” amesema Salum.

Kuhusu wateja waliopo, Salum amebainisha kuwa hivi karibuni MultiChoice itazindua promosheni kubwa na ya aina yake kwa wateja wake hivyo wakae mkao wa kula.