Mashabiki wa Simba wamshangaa kocha Aussems

Saturday May 11 2019

By OLIPA ASSA

SHUKRANI ya punda ni mateke! Ndio kauli unayoweza kuitoa kuelezea namna mashabiki wa Simba walivyowageuka wachezaji na benchi la ufundi jana Ijumaa wakiwatuhumu kwa uzembe uliopelekea wapoteze mechi yao dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mashabiki hao wachache waliojitokeza uwanjani wakionekana kuchukizwa na kiwango ambacho kilionyeshwa na wachezaji wao kwenye mchezo huo walioachapwa bao 1-0.

Katika mchezo huo wachezaji wa Simba walionekana kucheza taratibu na kuzidiwa katika kumiliki wa mpira na Kagera Sugar hasa kipindi cha kwanza jambo ambalo liliwafanya mashabiki wa timu hiyo kutoa lawama kwa wachezaji na benchi la ufundi kuwa limechangia hali hiyo.

Pengine hali ya uwanja ambao ulikuwa na utelezi uliotokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam, wachezaji wa Simba walishindwa kumiliki mpira mara kwa mara na kuna nyakati walijikuta wakidondoka jambo lililoonekana kuwaudhi mashabiki.

Mashabiki hao walikuwa wakishinikiza wachezaji wa Simba kuacha soka la taratibu kwa madai kuwa ndilo lilikuwa likichezwa na Kagera Sugar na kuongeza kuwa ndilo lilikuwa linasababisha timu hiyo isipate mabao.

Baada ya Kagera Sugar kupata bao ambalo liliamua mchezo lilitokana na uzembe wa beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ ambaye alijifunga wakati alipokuwa kwenye harakati za kuokoa hatari langoni mwake.

Advertisement

Mbali na kukerwa na wachezaji pia Kocha wa Simba, Patrick Aussems amejikuta kwenye wakati mbaya kwa mashabiki wake wakidai anapanga kikosi ambacho sio cha ushindi.

Advertisement