Mashabiki Yanga waondoka kinyonge Simba ikimchapa mwarabu

Muktasari:

  • Simba imecheza mechi hizo za Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi wao wakiwa Kundi D, pamoja na Klabu za Al Ahly ya Misri, JS Saoula ya Algeria na Vita ya Congo.

Dar es Salaam. Mashabiki wachache wa Yanga waliofika kushuhudia mchezo wa Simba na JS Saoula ya Algeria, walijikuta wakiondoka kinyonge baada ya Wekundu hao wa Msimbazi kuwachapa Waarabu mabao 3-0.
Mchezo huo ambao ni wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na Simba kuonyesha kiwango safi.
Uliwafanya mashabiki hao walioingia kwa 'mbwembwe' wakiwa wamevalia jezi za JS Saoula na kubeba bendela za Algeria na kukaa sehemu moja kwenye viti vya orenji.
Kasi yao ya ushangiliaji ilizidi kupungua kila baada ya dakika ya mchezo ilivyokuwa ikisonga kutokana na kiwango hicho walichokionyesha Simba.
Mabao matatu yaliyofungwa na Simba la kwanza la Emmanuel Okwi lililofungwa ndani ya dakika za nyongeza baada ya 45, kumalizika na yale mawili ya Meddie Kagere ya dakika ya 51 na 67 yaliwanyong'onyesha kabisa mashabiki hao.
Hata hivyo, katika mchezo huo ambao ulishuhudiwa na mashabiki wengi wa Simba lakini hawakuujaza uwanja, sehemu kubwa walikuwa ni wao.
Mashabiki hao walikuwa wameupamba uwanja kwa sare ya jezi zao za rangi nyeupe na nyekundu.