Mashabiki Simba washushwa presha ishu ya Mo

Thursday October 11 2018

 

Katika hatua nyingine, Makonda amewataka shabiki wa Simba na watanzania kuwa Wavumilivu wakati  Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi.
Hata hivyo, Haji Manara ambaye ni msemaji wa klabu hiyo ya simba hakuwa tayari kuzungumza. "inatosha alichokisema Makonda kwa shabiki wa Simba, inatosha,"amesema.
Pia ametoa onyo Kali Kwa watumiaji wa mitandao kutokuwa wazungumzaji Wa tukio hilo, na badala yake kusaidia Polisi utoaji wa taarifa.
Kuhusu utekaji Dar , Makonda amesema utendaji kazi wa Polisi unapimwa kwa hatua inazochukua Kila baada ya kupokea taarifa za tukio.
Amewataka wakazi wa jiji hilo kuwa na ushirikiano katika utoaji wa taarifa za matukio hayo kabla ya kutokea.

Advertisement