Mashabiki Simba wampaisha Maxime

Friday May 10 2019kocha wa Kagera Sugar, Mecky Mexime .

kocha wa Kagera Sugar, Mecky Mexime . 

By Imani Makongoro

Dar es Salaam. Saa chache kabla ya Simba kucheza na Kagera Sugar, mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi walimshangilia kocha wa Kagera Sugar, Mecky Mexime .

Mashabiki hao waliokuwa wamevaa jezi za rangi nyekundu na nyeupe ambayo ni rangi ya mabingwa hao watetezi walimshangilia Mexime wakimtaja kuwa ni kocha bora.

Tukio la mashabiki hao kumshangilia Mexime lilitokea baada ya timu yake kumaliza kupasha tayari kwa mchezo wao na Simba kwenye uwanja wa Uhuru , Dar es Salaam.

 Huku akicheka, Mexime hakuwajibu chochote zaidi ya kuwaonyeshea mikono kwa ishara ya kushukuru na kisha kuelekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza Simba ilifungwa mabao 2-1 kwenye uwanja wa Kaitaba Kagera.

Advertisement