Mashabiki Simba, Yanga Mwanza walianzisha mechi ya watani

Muktasari:

 

  • Moja ya sababu za mashabiki hao kutamba kuwa timu zao kushinda ni pamoja na ubora wa vikosi vyao namna vilivyo bora.

Mwanza.Wakati wadau wa Soka nchini wakisubiri kwa hamu mechi ya watani wa jadi, Yanga na Simba, jijini Mwanza tambo zimekuwa kali kwa kila upande ukisifia kikosi chake na kwamba ushindi ni lazima.

 Yanga na Simba zinakutana Jumamosi hii katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam, huku mchezo huo ukiwa unavuta hisia kubwa kwa mashabiki na wadau wa soka nchini.

 MCL Digital imepiga hodi katika matawi ya mashabiki wa timu hizo na kuzungumza na baadhi ya mashabiki wa klabu hizo ambapo kila mmoja ametamba kuwa lazima chama lake lishinde.

 Moja ya sababu za mashabiki hao kutamba kuwa timu zao kushinda ni pamoja na ubora wa vikosi vyao namna vilivyo bora.