Marco Verratti abwaga kitu, achukua kisu kingine matata kweli

Muktasari:

Mrembo Jessica amekuwa akiwatega wafuasi wake huko Insta kwa picha zake, huku shabiki mmoja wa peji yake, akiwahi kumuuliza kwamba anawezaje kuwa mrembo hivyo.

PARIS, UFARANSA . KIUNGO staa wa Paris Saint-Germain, Marco Verratti ni kama amewathibitishia tu watu kwa sasa yupo kwenye penzi moto la mrembo matata, Jessica Aidi.

Si unajua, fundi huyo wa mpira wa kimataifa wa Italia hivi karibuni aliachana na aliyekuwa mkewe, mrembo Laura Zazza, sasa ameangukia kwenye mahaba ya mwanamitindo wa Kifaransa, Jessica.

Wawili hao walionekana pamoja kwenye wiki ya mitindo huko Ufaransa na hapo kuanza kuamsha fununufununu Verratti ameshanasa na Jessica, ndiye aliyekuja kuziba pengo la Laura kwa kiungo huyo.

Kwanza kabisa, Verratti na mrembo Jessica walionekana pamoja wakiwa wameshikana mikono kwenye mashindano ya Monaco Grand Prix, Mei, licha ya kwamba wakati ule ilikuwa ngumu kuweka mambo hadharani.

Kinachoelezwa ni kwamba wawili hao walikutana, wakati Jessica, alipotuma kwenye mtandao wake wa kijamii kuhusu like ya Verratti ya jarida la Sports Illustarted - kipindi hicho mrembo huyo alipokuwa akifanya kazi ya uhudumu.

Baadaye, mambo yalikuwa moto baada ya Verratti kuthibitisha yeye na Laura wameachana. Verratti kwenye ndoa yake na Laura Zazza wamefanikiwa kupata watoto wawili, Tomasso na Andrea.

Hata hivyo, kiungo huyo wa zamani wa Pescara ibadi awe mvumilivu sana kwenye penzi jipya kutokana na kwamba mrembo Jessica amekuwa akikusanyia wafuasi wengi kwenye mtandao wa Instagram kutokana na picha zake za utata ambazo amekuwa akituma.

Mrembo Jessica amekuwa akiwatega wafuasi wake huko Insta kwa picha zake, huku shabiki mmoja wa peji yake, akiwahi kumuuliza kwamba anawezaje kuwa mrembo hivyo.

Mwingine alisema sasa amepata ufahamu mzuri kwanini Verratti hakuomboleza sana baada ya talaka kwamba moja kwa moja alikwenda kuzama kwenye penzi la mwanamke huyo.

Chama la Verratti kwa sasa linaongoza kwenye Ligi Kuu Ufaransa baada ya kushinda mechi saba kati ya tisa za kwanza ilizocheza hadi sasa, wakiwa wamekusanya pointi 21, wameshinda mechi saba na kuchapwa mbili, huku wakifunga mabao 17 na kufungwa manne tu.