Marcelo atoboa siri Ronaldo, Neymar

Saturday June 9 2018

 

Madrid, Hispania. Beki wa Real Madrid, Marcelo amefyumu na kufunguka kwamba Cristiano Ronaldo si mmiliki wa Real Madrid na kama anataka kuondoka sio ishu licha ya kwamba wachezaji wangependa sana abaki kwenye timu yao.

Ronaldo ameripotiwa kuchafua hali ya hewa huko Santiago Bernabeu baada ya kudai kwamba anaondoka kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya, huku akisema jambo hilo muda mfupi baada ya kubeba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuichapa Liverpool 3-1 huko Kiev, Ukraine.

Wiki hii mambo yamecharuka zaidi juu ya Ronaldo kuondoka huku madai yakielezwa kwamba ametibuana na rais Florentino Perez.

Alipoulizwa Marcelo anasema huu ya sakata hilo, alisema hivi: "Cristiano haimiliki Real Madrid, kama rais (Florentino Perez) anataka kusajili mtu, basi atasajili tu. Lakini, kwa sababu ya Cristiano...Neymar asije? Wachezaji wote wanamtaka Cristiano abaki, lakini Neymar naye siku zote milango ya Real Madrid ipo wazi. Real siku zote wanatazama wachezaji bora siku moja Neymar atakuja kuichezea Real Madrid."

 

Advertisement