Marcelo amchongea Bale Real Madrid

Muktasari:

Marcelo alisema Bale amekuwa akizungumza kingereza ndani ya vyumba vya kuvalia nguo badala ya Kihispania.

Madrid, Hispania.Marcelo amemchomea utambia Gareth Bale akidai licha ya kudumu katika kikosi hicho kwa miaka sita hajui Kihispania.

Beki huyo wa kushoto alisema mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Wales, amekuwa akizungumza lugha ya Kiingereza.

Marcelo alisema Bale amekuwa akizungumza kingereza ndani ya vyumba vya kuvalia nguo badala ya Kihispania.

Alisema Bale alipaswa kujua lugha ya Taifa hilo kwa kuwa ndiyo njia sahihi ya mawasiliano.

Bale alitua Real Madrid akitokea Tottenham Hotspurs mwaka 2013, lakini amekuwa akitumia lugha ya nyumbani kwao Uingereza.

Kauli ya Marcelo imekuja wakati kukiwa na taarifa kuwa mchezaji huyo anaweza kuondoka katika usajili wa majira ya kiangazi msimu ujao.

“Bale anazungumza lugha moja kingereza, anafahamu maneno mawili tu,” alisema beki huyo wa kimataifa wa Brazil.

Mshambuliaji huyo amefunga mabao 100 katika kikosi hicho ingawa maisha yake ndani ya klabu hiyo yako shakani licha ya kutajwa kwamba ndiye tegemeo la Real Madrid baada ya kuondoka Cristiano Ronaldo.