Maradona amchapa konde mwandishi wa habari Mexico

Muktasari:

  • Gwiji la soka kutoka Argentina, Diego Maradona, kwa mara nyingine ameshindwa kupata ufanisi katika kazi ya ukocha baada ya timu aliyokuwa akiinoa ya Dorados kushindwa kupanda daraja na kocha huyo kuamua kumaliza hasira zake kwa kutaka kuzichapa na mwadishi wa habari baada ya kumalizika mechi ya pili ya Fainali.

Mexico City, Mexico. Kocha wa timu ya Dorados, Diego Maradona aliamua kurusha ngumi kwa mwandishi wa habari aliyetaka kumpiga picha.

Maradona ambaye alikuwa uwanjani alikazimika kukaa jukwaani kutokana na kutumikia adhabu ya kutokaa kwenye benchi la fundi baada ya kulimwa kadi nyekundu katika mchezo wa kwanza wa mtoano.

Gwiji huyo kutoka Argengtina alikasirika baada ya timu yake kufungwa katika mchezo wa pili wa mtoano ambapo Dorados ilihitaji sare tu kuweza kupanda daraja.

Maradona alihamaki baada ya filimbi ya mwisho amba Dorados ilipoteza kwa jumla ya mabao 4-3 kutoka kwa Atletico San Luis.

Awali Maradona alikataa kuzungumza na vyombo vya habari na alipokatiza katikati ya wanahabari mmoja alitaka kumpiga picha ndipo akageuka mbogo.