Mapacha watatu original yahamishia majeshi Mwanza, kahama na Shinyanga

Wednesday September 18 2019

Mapacha watatu, original, yamishia, majeshi Mwanza, Mwanaspoti, Tanzania

 

By Rhobi Chacha

Dar es Salaam. Miaka mitatu tangu kuundwa kwa bendi ya Mapacha watatu original chini ya Khalid Chokora na mkewe Cathy Chuma inataraji kufanya ziara ya katika mikoa ya Mwanza, Kahama na Shinyanga.

Maonyesho hayo yaanza kufanyika mkoani Mwanza Ijumaa hii 20-09-2019, Jumamosi 21-09-2019 kundi zima la Mapacha watatu Original litakuwa mkoani Kahama kwa shughuli maalumu na watamalizia ziara kwa kufanya onyesho la nguvu  Shinyanga jumapili 22-09-2019 kwenye ukumbi wa La Prince Pub.

Bendi hiyo inataraji kuondoka na wanamuziki wake wote usiku wa leo Jumatano baada ya shoo Club Maisha Mwenge.

Mapacha watatu Original wanatumia ziara hii kwa ajili ya kutambulisha bendi yao inayotamba sasa hivi katika kumbi mbalimbali hapa Dar es Salaam ikiwa ni mara yao ya kwanza kutoka nje ya mji na nyimbo kama Nyumba ndogo,Yananitesa, Private Case, Kipaji changu, Shika Ushikapo, Sumu ya Mapenzi,Usia wa Babu,Kuachwa na nyingine nyingi.

Mapacha watatu Original itarudi Jijini Dar es salaam  Jumatano tarehe 25-09-2019 kwa ajili ya shoo siku hiyo katika ukumbi wa Club Maisha uliopo Mwenge.

Ziara hii ni mfululizo wa mkakati wa Mapacha watatu Original wa kufanya ziara kwa ajili ya maonyesho maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuzidi kujitangaza, kabla ya kwenda mikoa ya kanda ya Ziwa Mapacha watatu Original imeshafanya maonyesho mengi katika  jiji la Dar es Salaam Last Minute Bar Sinza Mori Kwa Irene Uwoya muigizaji wa Bongo Movies, Forty Forty Bar Tabata,Life Terrace zamani new Word Cinema Mwenge,Kisuma Bar Magomeni,na nyingine nyingi.

Advertisement

 

 

 

Advertisement