Mandzukic kutua Old Trafford kwa Pauni 10 milioni

Muktasari:

Inamaaninika kwamba, Mandzukic ni anaweza kuwa tiba ya muda mrefu kwenye safu ya ushambuliaji ya timu hiyo ya Old Trafford.

MANCHESTER United italazimika kutoa kiasi cha Pauni 10 milioni kwa ajili ya kumchukua mshambuliaji wa Juventus, Mario Mandzukic katika dirisha la Januari lakini tayari ina makubaliano na staa huyo wa kimataifa wa Croatia.

Kocha wa United, Ole Gunnar Solskjaer anapambana kupata mshambuliaji mahiri katika dirisha la Januari baada ya kudorora kwa safu yake ya ushambuliaji baada ya kuumuza Romelu Lukaku huku akimtoa kwa mkopo Alexis Sanchez.

Inamaaninika kwamba, Mandzukic ni anaweza kuwa tiba ya muda mrefu kwenye safu ya ushambuliaji ya timu hiyo ya Old Trafford.

Man United imekuwa ikiwategemea Marcus Rashford ambaye amecheza mechi nane za Ligi Kuu na kufunga mabao matatu tu, Mason Greenwood aliyecheza michezo sita na hakutoka na bao, wakati Antony Martial amecheza michezo mitatu na kufunga mabao mawili na asisti moja tu kwenye Ligi Kuu England.