Manchester United yampa Rashford muda autakao kukaa nje

Muktasari:

Kocha wa Manchester United ameshindwa kuweka wazi kuhusu Rashford kurejea kama ni kabla ya mwisho wa msimu au wakati wa mashindano ya Euro 2020.

London, England. Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema watampa Marcus Rashford "muda mrefu anaotaka" ili kupoka kabisa majeraha yake.

Muda ambao Rashford atakosekana uwanja kutokana na majeruhi hayo haujulikani.

Kocha wa Manchester United ameshindwa kuweka wazi kuhusu Rashford kurejea kama ni kabla ya mwisho wa msimu au wakati wa mashindano ya Euro 2020.

Solskjaer amesama itachukua wiki sita kabla ya mshambuliaji huyo mwenye miaka 22 kurejea kuanza mazoezi.

"Marcus atakaa nje kwa muda atakaotaka yeye," alisema Solskjaer. "Hatutaki kuhatarisha maisha yake kwa sababu ya kuwa majeruhi. Wakati atakaporudi atakuwa fiti kwa asilimia 100%."

Solskjaer alilaumiwa na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na England, Ian Wright kwa uamuzi wa kumchezesha Rashford katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Wolves kwenye Uwanja wa Old Trafford wakati akijua ni majeruhi.