Manchester United yadaiwa kumnasa Kalidou Koulibaly

Muktasari:

Mwandishi wa habari wa Italia, Fabio Santini amefichua taarifa hizo alipozungumza kwenye kipindi cha televisheni cha Il Processo aliposema Napoli itampiga bei Koulibaly kwenda Man United kwa ada ya kati ya Euro 70 milioni hadi Euro 75 milioni na kinachoonekana dili limeshafika patamu.

MANCHESTER United imedaiwa kukamilisha dili la kumsajili beki wa kati wa Napoli, Kalidou Koulibaly kwa mkwanja unaozidi Pauni 60 milioni.

Koulibaly amehusishwa pia na Tottenham na Arsenal, lakini kwa mujibu wa taarifa za kutoka Italia, Man United imefanya haraka kuinasa saini yake. Hata hivyo, beki huyo hatajiunga na timu yake mpya Januari, atasubiri hadi mwishoni mwa msimu, huku saini yake ikidaiwa itakuwa kitu muhimu kwenye kuimarisha beki ya wababe hao wa Old Trafford.

Mwandishi wa habari wa Italia, Fabio Santini amefichua taarifa hizo alipozungumza kwenye kipindi cha televisheni cha Il Processo aliposema Napoli itampiga bei Koulibaly kwenda Man United kwa ada ya kati ya Euro 70 milioni hadi Euro 75 milioni na kinachoonekana dili limeshafika patamu.

Kwa muda mrefu sasa mashabiki wa Man United wamekuwa wakilialia kutaka timu yao ijasajili beki mwingine wa kati wa kiwango cha dunia kwenda kuungana na beki wao Harry Maguire.