Man United yamkera wakala wa Van de Beek

 Manchester, England. Kiungo mpya, Donny van de Beek hajaanza katika mchezo wowote wa Ligi Kuu England hadi sasa tangu kujiunga na Manchester United akitokea Ajax, jambo lililomkera wakala, Sjaak Swart.

Akizungumza na mtandao wa VoetbalPrimeur, Swart alisema: “Kutokea benchi, suala hili silipendi hata kidogo. Hata mimi binafsi siwezi kulifanya, anasimamishwa zikiwa zimebaki dakika nne.”

Kiungo huyo wa kimataifa wa Uholanzi alijiunga na Man United kwa uhamisho wa Pauni 40 milioni, mashabiki wamekuwa wakitamani kumwona akicheza sambamba na Bruno Fernandes na Paul Pogba. Hata hivyo, alionekana akiingia katika mechi zao mbili za ligi, akicheza kwa dakika 23 dhidi ya Crystal Palace na akiingia pia dakika za mwisho katika mchezo dhidi ya Brighton.

Mchango wake ulikuwa mkubwa katika michezo yote, alifunga katika mchezo dhidi ya Palace na pia alisababisha penalti katika mchezo dhidi ya Brighton, wakati Man United ilizamishwa sare.

“Alifanya vitu vitatu zaidi vizuri,” alisema Swart. “Penalti, ambayo walipata bao la tatu, lilitokea kwake. Wangeweza kufungwa hata mabao 7-1. Brighton waligongesha nguzo mara tano. Wana timu nzuri, lakini halitakiwi kutokea kwa Manchester United.”