Man United yamfukuzia beki kisiki kinda kutoka Ghana

Muktasari:

Salisu ameibuka kuwa mmoja kati ya walinzi wa nguvu katika soka la Hispania huku akianza kusakwa na klabu mbalimbali kubwa, na Manchester United wanaongoza katika mbio za kumsaka huku kipengele chake cha mauzo kikiwa ni Pauni 20 milioni.

MANCHESTER United imepokea habari njema kutoka katika klabu ya Real Valladolid ya Hispania baada ya kuambiwa kwamba mlinzi nyota wa timu hiyo, Mohamed Salisu, 20, amegoma kusaini mkataba mpya na anaweza kuuzwa kwa bei chee.

Salisu ameibuka kuwa mmoja kati ya walinzi wa nguvu katika soka la Hispania huku akianza kusakwa na klabu mbalimbali kubwa, na Manchester United wanaongoza katika mbio za kumsaka huku kipengele chake cha mauzo kikiwa ni Pauni 20 milioni.

Salisu mwenyewe ameng’ang’ania kuondoka Hispania kwa ajili ya kwenda Ligi Kuu ya England na United wamegundua kwamba mlinzi huyo mrefu na mwenye nguvu atawasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa matatizo katika safu ya ulinzi. United inawategemea zaidi walinzi iliowasaji msimu huu akina Harry Maguire na Aaron Wan-Bissaka, lakini inahitaji mchezaji mwingine kusaidia eneo la ulinzi.