Man United yaendeleza ubabe UEFA

Muktasari:

Man United ndio inaongoza kwenye msimamo wa kundi H, ikiwa na alama sita baada ya kucheza mechi mbili na kushinda zote.

MANCHESTER, ENGLAND. MABAO ya  Mason Greenwood, Anthony Martial na Marcus Rashford aliyefunga Hat Trick ndio yameifanya Manchester United kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya RB Leipzig kwenye muendelezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, jana katika uwanja wao wa nyumbani.

 

Baada ya mchezo huo kocha wa Man United alisema timu yake ipo vizuri kwa sasa na  kiwango hicho kinampa nafasi ya kuamua nani acheze kwa sababu wachezaji wote wanaokena kupigana katika dakika zote 90.

 

 

Lakini licha ya viwango vilivyooneshwa na wachezaji wa safu ya ushambuliaji Solskjaer hakuacha kuwamwagia sifa kwa viungo wake hususani Mbrazil Fred.

 

" Nafikiri hakuna sehemu ya Uwanja ambayo hakukanyaga. Alionekana kwenye mipira yote, kiufupi nimpongeze kwa jitihada kubwa alizofanya katika muda wote aliocheza na hakuonyesha kuchoka hata kidogo. Kiwango  alichoonesha kilikuwa zaidi ya nilivyotegemea," alisema.

 

Ushindi huo unakuwa wapili kwa Man United katika michuano hiyo baada ya mchezo wa kwanza kuibamiza PSG mabao 2-0, kwenye mechi ya ufunguzi ya kundi H.

 

Man United ilianza na viungo wanne kwenye ambapo kiungo wa chini alikuwa ni Nemanja Matic. Pogba na Fred wakawa wanacheza kati kati huku Donny van de Beek akicheza kama kiungo mshambuliaji mfumo ambao ulionekana kuifaidisha zaidi kwenye mchezo huo.

 

Mchezo ujao Man United itakuwa nyumbani kuumana na Arsenal katika muendelezo wa Ligi Kuu ikiwa ni miongoni mwa mechi ambazo mashabiki wa timu hiyo wanazisubiria kwa hamu kubwa kutokana na aina ya matokeo ambayo timu hiyo imekuwa nayo katika michezo mitatu ya mwisho.