Man United wapewa Barcelona robo fainali Uefa

Muktasari:

Madrid chini ya Kocha Zinedine Zidane imechukua mara tatu
mfululizo na alipoondoka tu, ikaanza kutetereka kwa kupata
matokeo mabaya.

Droo ya robo fainali ya Klabu Bingwa Bara la Ulaya (Uefa Champion League) imefanyika leo Ijumaa Nyon, Uswisi ambapo mechi kali inatajwa kuwa kati ya Barcelona na Manchester United.


Manguli hao wa soka barani Ulaya watacheza mchezo wa kwanza
katika Uwanja wa Old Trafford, England na Manchester United
atakuwa mwenyeji siku ya Aprili 9, ambayo itapigwa michezo yote minne.


Mechi nyingine Liverpool atawakaribisha FC Porto kwenye Uwanja
wa Anfield, Ajax itakuwa nyumbani kukipiga na Juventus wakati
Tottenham Hotspour watakuwa wenyeji wa Manchester City na mechi hizo zitachezwa nyumbani na ugenini.


Katika michuano hiyo, Real Madrid ambao ndio mabingwa watetezi, waliyaaga mapema mashindano hayo.


Madrid chini ya Kocha Zinedine Zidane imechukua mara tatu
mfululizo na alipoondoka tu, ikaanza kutetereka kwa kupata
matokeo mabaya.


Siku tatu zilizopita, Real Madrid imemrudisha nyumbani Zinedine
kuendelea na majukumu yake.