Man United imekula za uso

BIRGNGHAM, ENGLAND. KAPTENI wa Aston Villa Jack Grealish ambaye juzi alisaini mkataba wa miaka mitano kuendelea kuitumikia Villa na amesema kuwa kusaini mkataba mpya kumemfanya kuwa na furaha, hiyo inatokana na mipango ambayo viongozi wake wameiandaa kwa msimu huu.

Mchezaji huyo ni miongoni mwa viungo ambao United ilikuwa inatamani kuwasainisha katika dirisha hili, lakini kusaini kandarasi mpya ya muda mrefu kumefanya matumaini hayo kupotea.

Grealish mwenye umri wa miaka 25, alisema ni kweli kulikuwa na ofa nyingi kutoka klabu za EPL na ligi nyingine, lakini maamuzi yake ilikuwa ni Villa kwa sababu anatamani kucheza hapo.

“Viongozi walinifata na kunieleza nini malengo yao kwa msimu ujao na nilipenda ndio nikaamua kusaini, najisikia furaha sana kuendelea kuwa hapa na hilo nimekuwa nalisema kila siku, Villa ni klabu iliyokaribu na familia yangu pia,” alisema.