Man City wadai Man United inafanya fitna

Thursday May 16 2019

 

MANCHESTER, ENGLAND.MANCHESTER City inaamini kuna kampeni inayofanywa na klabu kubwa Ulaya wakiwamo mahasimu wao Manchester United ili kuwarudisha nyuma.

Man City imekuja mbogo baada ya kuwapo kwa ripoti huenda wakakumbana na adhabu ya kufungiwa kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Kamati ya nidhamu ya Uefa imedaiwa huenda akaifungia Man City kucheza Ligi ya Mabingwa kwa mwaka mmoja kama itakutwa na hatia ya kukiuka kwenye sheria ya uwiano wa matumizi ya pesa na mapato kwenye klabu hiyo.

Manchester City inadai takwimu za matumizi ya pesa zilizopelekwa Uefa ni za uongo huku wakidai kuna fitna.

Advertisement