Mamilioni ya SportPesa yabebwa Lucumay

Wednesday April 24 2019

 

By Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa imeendelea kuwapa mzuka watanzania kwa kumwana mamilioni ya fedha kupitia jackpot yake.

Jackpot hiyo kwa sasa imefika Sh 624.2milioni ambapo, unaweza kushinda kwa sh 2000 tu mshiriki anaondoka na mamilioni hayo kama atabashiri kwa usahihi mechi zote 13.

Kwa wiki hii bahati imekwenda kwa mkazi wa Biharamulo mkoani Kagera, Ibrahim Godwin Lucumay, ambaye amebashiri na kupatia mechi 12 kati ya 13 na kujinyakulia bonasi ya sh43.1 milioni.

“Nilivutiwa kucheza na SportPesa ni malipo papo hapo. Siku moja nilicheza multibet ya SportPesa na walinilipa baada ya mechi ya mwisho kuisha, lakini kwingine nilipata baada ya siku mbili kupita.

“Tangu wakati huo nimekuwa nikicheza na SportPesa tu kwa sababu inanipa uhakika na hasa Jackpot imefikia milioni 200 ambayo haipo kwenye kampuni zingine.

“Matarajio yangu baada ya ushindi huu ni kuongeza kipato kwenye biashara, kwa kweli SportPesa imebadilisha maisha yangu,” anasema Lucumay.

Advertisement

Kwa upande wa SportPesa Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti, Tarimba Abbas alimpongeza Lucumay kwa kucheza bila kukata tamaa na hatimaye kubeba mamilioni hayo.

“Huduma zetu kama alivyosema Lucumay ni za haraka na mchezo unapokwisha tu pesa huwekwa kwenye akaunti ya SportPesa papo hapo, lengo ni kuhakikisha huduma zetu zitatolewa kwa wakati,” alisema Tarimba huku akiwahamasisha Watanzania kushiriki kwa wingi ili kuboresha maisha.

 

Advertisement