Mambo manne yaliyoipeleka Yanga kileleni

Muktasari:

  • Ushindi huo umewafanya Yanga kurejea kileleni wakiwa na pointi 83 katika michezo 36 waliyocheza, huku Simba wakishika nafasi ya pili wakiwa na pointi 82 katika michezo 33 waliyocheza.

KLABU ya Yanga imefanikiwa kurejea katika nafasi ya kwanza baada ya kuichapa Ruvu Shooting bao 1-0 katika mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Ushindi huo umewafanya Yanga kurejea kileleni wakiwa na pointi 83 katika michezo 36 waliyocheza, huku Simba wakishika nafasi ya pili wakiwa na pointi 82 katika michezo 33 waliyocheza.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa kukatana shoka, Yanga waliweza kutumia makosa machache ambayo yaliweza kuipa ushindi mbele ya Shooting.

Mwanaspoti linakuletea uchambuzi mfupi namna ambavyo Yanga walivyoweza kupata ushindi huo na kurejea kileleni na kuishusha Simba.

KUTOKATA TAMAA

Licha ya kwamba Yanga imekua ya kuunga unga huku mashabiki wao wenyewe wakiwa wanalitambua hilo, kwa upande wa wachezaji wao hawajawahi kukata tamaa.

Wachezaji wa Yanga wanapokuwa wanacheza mechi huwa wanapambana dakika zote ambazo wanakuwa uwanjani, hali ambayo inawafanya wapate matokeo mazuri.

Katika mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting, tangu filimbi inapigwa sekunde ya kwanza walionyesha kabisa hawana cha kupoteza katika mchezo huo zaidi ya ubingwa.

Kila mchezaji alikuwa anahangaika kuhakikisha analisogelea goli la Shooting na waliweza kufanikiwa mapema tu baada ya dakika 18, Papy Tshishimbi kuifungia goli lillilodumu mpaka dakika 90.

Baada ya goli hilo Yanga hawakuonyesha kulizika kwani walikuwa wakikaba na kushambulia, hata hivyo Shoooting nao walikuwa wanajibu mapigo lakini walikuwa wanakutana na changamoto kutoka kwa mabeki wa Yanga ambao walikuwa hawataki kabisa mpira ukae kwao.

SHOOTING HAWAKUIHESHIMU YANGA

Kocha Abdulmutic Haji wa Ruvu Shooting aliingia katika mchezo huo akiwa na lengo la kutoka sare katika kipindi cha kwanza na kipindi cha pili kufunguka.

Hata hivyo Yanga waliotea mtego huo na bao la mapema la Tshishimbi liliwavuruga vilivyo wachezaji wa Shooting, kwani walionekana kuanza kucheza kwa presha kubw sana.

Yanga walizidisha utulivu na kufanya mashambulizi ya kwa kutumia mawinga wao wa pembeni kitu (Mwinyi Haji na Juma Abdul) ambao walikuwa wanapiga krosi ambazo zilionekana kuleta faida kwa upande wao.

Kitendo cha kufunguka kwa Shooting kuliwafanya wakoswe magoli mengi katika kipindi cha pili kwani Yanga waliamua kufanya mabadiliko kwa kumuingiza Ajib ambaye aliweza kuendana na kasi ya mchezo huo.

SHOOTING WALIKOSA MSHAMBULIAJI MATATA

Katika mchezo huu Ruvu Shooting walikuwa kama wamejifunga baada ya kufunguka na kushambulia, lakini walikuwa hawana mtu wa kusimama juu karibu na goli.

Shooting walikuwa wanamtumia Full Maganga,lakini alionekana mapema kwamba mchezaji huyo amecchoka na kushindwa kupigana vikumbo na wachezaji wa tikmu pinzani.

Kama wangekuwa na mshambuliaji mwingine ambaye ana udambwi dambwi  angewezaa kusaidiana na Maganga bila shaka wangeweza kupata goli la kufutia majonzi.

Safu ya ulinzi haikuwa vizuri sana kwani walikuwa wakutumia mipira ya ngujvu kwa pasi za chini.

KUMKAMIA MAKAMBO KUMEMPONZA

Makambo hivi sasa amezidi kukaziwa na mabeki wa timu pinzani kitu ambaacho kimemfanya aendelee kusalia na magoli yake 16 huku Meddie Kagere akizidi kuchanua baada ya kufikisha magoli 20.

Katika mchezo huu dhidi yaa Shooting mabeki wa Shooting walikuwa wakitembea jino kwa jino na Makambo kitu ambacho kiliwaingi za mkenge kabisa.

Kwani Yanga walikuwa wakiwatumia wachezaji wake wote katika kushambulia ili kuweza kupata goli la kuongoza