Malale, Polisi kimeeleweka

Muktasari:

Mwenyekiti wa Timu hiyo, Charles Mkumbo alisema baada kupitia wasifu wa makocha waliomba kazi kwenye kikosi hicho, Malale ndio alikidhi vigizo walivyokua wanavihitaji.

Uongozi wa Polisi Tanzania, umemsainisha, Malale Hamsin mkataba wa mwaka mmoja kuziba nafasi ya Seleman Matola aliyetimkia Msimbazi.
Mwenyekiti wa Timu hiyo, Charles Mkumbo alisema baada kupitia wasifu wa makocha waliomba kazi kwenye kikosi hicho, Malale ndio alikidhi vigizo walivyokua wanavihitaji.
"Tunajua uwezo wa Malale katika timu za Ligi Kuu alizopita, tunauhakika atafanya makubwa kwenye timu yetu katika mashindano mbalimbali ikiwemo FA," alisema Mkumbo.
Kwa upande wake Malale alisema anaomba Ushirikiano kutoka kwa uongozi pamoja na wachezaji ili kutimiza malengo ya timu.
"Siku zote Ushirikiano ndio unamfanya mtu kufanikiwa kwenye kazi yake, sina kitu cha kuwaahidi wapenzi wa Polisi zaidi ya kuhakikisha anafanya kazi kwa uwezo wake."