Makipa Simba utamu umenoga

Muktasari:

Akizungumza na Mwanaspoti, Mharami alisema anajivunia kuwa na makipa watatu ambao wote wana viwango vya hali ya juu jambo linalofanya kuwa na imani juu ya uimara wa eneo hlo kulekea msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na hata michuano ya kimataifa.

KIKOSI cha Simba kinaendelea kujifua kwa ajili ya mechi yake ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo Jumapili hii, lakini huko Gymkhana kunakofanyikia mazoezini hayo, utamu umenoga kwa makipa wa timu hiyo.

Aishi Manula aliyekuwa majeruhi amerejea na kuonyeshana kazi na Beno Kakolanya na Ally Salim, kitu ambacho kimempa mzuka kama wote kocha wao, Mohammed Muharami ‘Shilton’, aliyekiri anakunwa na ushindani wa makipa hayo kikosini kwa sasa.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mharami alisema anajivunia kuwa na makipa watatu ambao wote wana viwango vya hali ya juu jambo linalofanya kuwa na imani juu ya uimara wa eneo hlo kulekea msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na hata michuano ya kimataifa.

“Kwa sasa langoni mwa Simba tuko vizuri kwa asilimia zote maana Aishi tayari ameungana na wenzake katika mazoezi na wote viwango vyao vinawaruhusu kucheza mechi ya aina yeyote,” alisema kipa huyo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania aliyewahi kucheza soka lwa kulipwa Msumbiji na kuongeza;

“Ushindani wa namba uliopo hapa haumhusishi Manula na Kakolanya pekee, bali hata Ally naye ana uwezo wa kuwaweka benchi wenzake na hii ndivyo inavyotakiwa,” alisema.

Kipa huyo wa zamani wa Simba na Taifa Stars, alisema yeye hatengenezi ushindani ila mbinu anazowapa na kujituma kwao kumewafanya kuwe na mchuano mkali kiasi kwamba anakuna kichwa juu yao.

Kipa chipukizi, Ally Salim kwa upande wake alisema kwa namna ushindano ulivyo kikosini hakuna mwenye shida ya nani acheze au nani asicheze, bali wanajiweka fiti kwa michezo yote ijayo, kwa kutambua yeyote ana nafasi mbele ya makocha wao.

“Sisi hatuliangalii sana anayepangwa, kwa maana wote ni timu moja, tunachojali ni kupiga tizi na kujiweka fiti ili hata ukipewa nafasi isionekane tofauti na kipa mmoja hadi mwingine,” alisema Salim ambaye msimu uliopita alikuwa akichuana na Manula, Deo Munishi ‘Dida’, Said Mohammed ‘Nduda’ na Emmanuel Mseja.