Makapu aangua kilio Uwanjani Yanga ikiambulia pointi moja Moro

Muktasari:

Adeyum Salehe ndiye aliyeiokoa Yanga baada ya kufunga bao dakika ya 82 lililoamsha shangwe kwa mashabiki wa klabu hiyo waliohudhuria mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Haikufahamika chanzo cha Makapu kulia lakini wengi wanadhani ni kutokana na kusababisha bao la Mtibwa Sugar dakika ya 28, baada ya kudondoka chini na kupokonywa mpira na Salum Kihimbwa ambaye alimpasia Chanongo ambaye nae aliutumbukiza wavuni.

Yanga ilibidi kusubiri mpaka dakika za mwisho na kusawazisha bao lililowaokoa kulala mbele ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Adeyum Salehe ndiye aliyeiokoa Yanga baada ya kufunga bao dakika ya 82 lililoamsha shangwe kwa mashabiki wa klabu hiyo waliohudhuria mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Kama Mtibwa ingekuwa makini basi ingeweza kupata mabao mengi zaidi kipindi cha kwanza kutokana na kiwango ilichokionyesha kwani iliwabana Yanga ambayo haikuweza kupiga hata shuti moja lililolenga lango katika kipindi hicho.

Dakika ya 36 Chanongo alikosa bao la wazi baada ya kupiga shuti lililodakwa na Kabwili kabla ya Yanga nao kukosa bao dakika ya 45 baada ya Adeyum kupiga faulo iliyookolewa na wachezaji wa Mtibwa Sugar.

Mabadiliko yaliyofanywa na kocha wa Yanga,Luc Eymael kwa kuwatoaLamine Moro aliyeumia,David Molinga na Abdulaziz Makame na kuwaingiza Ditram Nchimbi Mrisho Ngassa na Tariq Seif, yalisaidia kuichangamsha Yanga na kurejea mchezoni hivyo kuwapa wakati mgumu Mtibwa Sugar hasa dakika 20 za mwisho za kipindi cha pili.

Hata hivyo katika

Katika michezo mingine KMC ililala kwa bao 1-0 mbele ya Prisons katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.Bao la washindi lilifungwa na Ramadhan Ibata wakati kwenye Uwanja wa Karume Musoma, Mwadui waliichapa Biashara United bao 1-0.

Kwenye Uwanja wa Namfua Singida, Kagera Sugar waliibamiza  Singida United mabao 2-1. Mabao ya washindi yalifungwa  na  Kelvin Sabato na Awesu Awesu wakati la wenyeji lilifungwa na Steven Opoku wakati kwenye  Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, wenyeji Mbao waliifanyia mauaji Namungo kwa kuichapa mabao 3-0 yaliyofungwa na Jordan John aliyefunga mawili na Abdulkarim Segeja.