Yanga yapata pigo! Makamu mwenyekiti kamati ya mashindano afariki dunia

Muktasari:

Mtoto wake wa kiume, Nasri Urungu amesema baba yake amefariki dunia akiwa nyumbani kwake Temeke, jijini Dar es Salaam baada ya presha kushuka.

Dar es Salaam. Taarifa mbaya kwa Yanga ni kwamba makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Mustapha Urungu amefariki dunia mchana wa leo Jumamosi.

Taarifa zilizothibitishwa na mtoto wake wa kiume, Nasri Urungu amesema baba yake amefariki dunia akiwa nyumbani kwake Temeke, jijini Dar es Salaam baada ya presha kushuka.

Nasri amesema awali baba yake aliamka akiwa sawa lakini ghafla mchana leo alizidiwa na kufariki dunia.

Mbali na kuwa makamu mwenyekiti wa kamati ya mashindano pia alikuwa makamu wa kamati ya usajili ya klabu hiyo.