Makambo kazidiwa bwana

Muktasari:

  • Makambo ndiye aliyekuwa kinara kabla ya kulingana na Aiyee na kisha kupitwa kwa bao moja.

KIWANGO bora cha mshambuliaji wa Mwadui, Salim Aiyee kimeanza kuwaibua wadau mbalimbali wa soka wakianza kuonyesha kuvutiwa na namna anavyocheza na kuwakimbiza hadi mapro wa kigeni waliosajiliwa kwa mbwembwe nchini.

Juzi Jumanne, Aiyee alitupia mabao mawili na kumfanya afikishe jumla ya mabao 13 na kuwa kinara wa wafungaji katika Ligi Kuu Bara akimzidi straika wa Yanga, Heritier Makambo mwenye mabao12 baada ya kuitungua Mbao jana Jumatano.

Makambo ndiye aliyekuwa kinara kabla ya kulingana na Aiyee na kisha kupitwa kwa bao moja.

Kocha Mkuu wa Mwadui, Ally Bizimungu alisema kujituma kwa mchezaji huyo ndio chanzo cha mafabikio.