Makambo hatihati mechi ya Biashara

Saturday December 8 2018

 

By Oliver Albert

Dar es Salaam.Kocha wa Yanga Mwinyi  Zahera amesema mchezo was kesho dhidi ya Biashara United utakuwa mgumu  lakini watapambana kuhakikisha wanapata pointi tatu na kuendelea kuongoza ligi.
Hata hivyo Zahera alisema anaweza kumkosa mshambuliaji wake Herieter Makambo ambaye alipata majeraha kidogo ya mguu katika mazoezi leo Jumamosi asubuhi.
"Mechi itakuwa ngumu kwani tunakutana na timu ambayo iko mkiani hivyo itatukabili kwa nguvu kwani inataka ipate matokeo na kuzidi kujiimarisha kwenye msimamo wake ligi
"Lakini hata sisi tunataka kuendeleza rekodi yetu ya ushindi na kuendelea kubakia kileleni.
Zahera alisema katika mchezo huo atawakosa Mrisho Ngassa mwenye kadi nyekundu na Ibrahim Ajib mwenye kadi tatu za njano na pia ana msiba.
"Pia Makambo yuko nusu nusu kucheza itategemea na matibabu atakayopata na ripoti ya daktari kwani alipata majeraha kidogo asubuhi kwenye mazoezi hivyo tunaendelea kumuangalia mpaka kesho nitajua Kama atacheza au la" alisema Zahera.

Advertisement