Makambo aanza kazi Haroya AC

Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga Heritier Makambo (kulia) akiwa katika picha maalum ya utambulisho kwenye klabu yake mpya ya Horoya AC, katikati ni winga wa zamani wa Azam FC  Enock Atta na kushoto ni mshambuliaji Aristide Bance

Muktasari:

Horoya pia imemtambulisha mshambuliaji mkongwe Aristide Bance akitokea Al Masry ya Misri.

ALIYEKUWA mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo ametambulishwa rasmi na klabu yake ya Horoya AC ya Guinea na kuanza kazi.
Makambo ameanza kazi baada ya Yanga kumalizana na Horoya na kukamilisha taratibu za uhamisho uliogharimu zaidi ya Euro 70,000.
Katika utambulisho huo Makambo raia wa DR Congo ametambulishwa sambamba na winga wa zamani wa Azam FC, Enock Atta.
Atta alivunja mkataba na Azam  kisha siku chache baadaye alisajiliwa na Horoya AC.
Horoya pia imemtambulisha mshambuliaji mkongwe Aristide Bance akitokea Al Masry ya Misri.
Wachezaji hao wote wamefanya mazoezi yao ya kwanza wakiwa na Horoya ambao ni Mabingwa wa Ligi Kuu ya Guinea wakijiandaa na msimu mpya.