Mahrez atingisha kiberiti Manchester City

Muktasari:

  • Mahrez ambaye ni mchezaji ghali zaidi Manchester City akiwa amenunuliwa kwa dau la Pauni 60 milioniameanza mechi 13 tu msimu huu huku mechi nyingi akitokea katika benchi na amekuwa haridhishwi na hali hiyo.

WINGA wa Manchester City, Riyad Mahrez ametishia kuondoka klabuni hapo huku akilalamika muda mchache anaopewa kucheza na kocha wa timu hiyo, Pep Guardiola ikiwa ni msimu mmoja tangu atue klabuni hapo akitokea Leicester City.

Mahrez ambaye ni mchezaji ghali zaidi Manchester City akiwa amenunuliwa kwa dau la Pauni 60 milioniameanza mechi 13 tu msimu huu huku mechi nyingi akitokea katika benchi na amekuwa haridhishwi na hali hiyo.

Mpaka sasa Mahrez amefunga mabao sita na kupika mengine matatu katika mechi 26 za Ligi Kuu England alizocheza na mpaka sasa ameshindwa kurudia makali yake yaliyomfanya kuwa mchezaji bora wa msimu wakati Leicester City ikitwaa ubingwa mwaka 2016, na sasa mambo yameanza kunda sivyo.