Maelfu ya mashabiki wa Manchester City wamuaga Kompany

Muktasari:

  • Kompany alisajiliwa na aliyekuwa kocha wa Man City, Mark Hughes mwaka 2008 akitokea Hamburg na ametwaa jumla ya mataji 10.

London, England. ya Maelfu mashabiki wa klabu ya Manchester City wamejitokeza mitaani kumuaga nahodha wao Vincent Kompany.
Kompany alitumia fursa ya mapokezi yao katika mitaa ya Manchester na London kutoa neno la mwisho baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka 11.
Nguli huyo mwenye miaka 33, anaondoka Man City baada ya kucheza kwa mafanikio makubwa tangu alipojiunga na klabu hiyoa mwaka 2008 akitokea Hamburg ya Ujerumani.
“Nataka niwaambie jinsi nilivyokuwa na furaha. Siwezi kujutia uamuzi wangu. Nimeipa klabu kila kitu, kudumu ndani ya klabu miaka 11 ni safari ndefu. Hatukuwa na mataji, lakini sasa tuna mataji, najivunia,” alisema Kompany.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji, ametangaza kurejea timu yake ya kwanza Anderlecht akiwa kocha mchezaji.
Mashabiki wanaokadiriwa kufikia 100,000 walijitokeza mitaani kutoa pongezi kwa wachezaji wa Man City kwa kazi nzuri waliyofanya msimu huu.
Kompany alisajiliwa na aliyekuwa kocha wa Man City, Mark Hughes mwaka 2008 akitokea Hamburg na ametwaa jumla ya mataji 10.