Madrid yatenga Pauni 187milioni za kumngoa Salah

Muktasari:

Wakati Madrid ikimnasa Eden Hazard dirisha lililopita la majira ya kiangazi, ilikwama kuwachukua Paul Pogba na Neymar ambao waligomewa na timu zao.

RAIS wa Real Madrid, Florentino Perez amemtambua winga wa Liverpool, Mohamed Salah kuwa ni mchezaji mwafaka wa kusajiliwa Santiago Bernabeu.

Wakati Madrid ikimnasa Eden Hazard dirisha lililopita la majira ya kiangazi, ilikwama kuwachukua Paul Pogba na Neymar ambao waligomewa na timu zao.

Hata hivyo, taarifa kutoka Hispania, Perez ameanza mipango ya mwakani kuboresha kikosi hicho, ambapo kwenye rada amewaweka Kylian Mbappe na Harry Kane huku akiamini atatua kunasa saini ya Salah mwishoni mwa msimu huu. Kwenye mpango huo, Perez ameandaa kiasi cha Pauni 187 milioni kumng’oa supastaa huyo wa Misri Anfield.

Jambo hilo linadaiwa litaibua vita kali kwa sababu Liverpool haitamruhusu aondoke baada ya kiwango bora anachokionesha, akishinda Kiatu cha Dhahabu kwenye Ligi Kuu England kwa misimu miwili mfululizo na wala hawana hofu kwa sababu mkataba wake bado unabakiza miaka zaidi ya mitatu.