Mademu wanaobeba mastaa Ulaya

Muktasari:

  • Messi kama kawaida anatarajia kuwa na sapoti kutoka kwa mrembo wake, Antonella Roccuzzo, huku Griezmann akisubiri kupata sapoti ya kutoka kwa mrembo wa nguvu, Erika Choperena na Mo Salah atakuwa na shangwe za kushangiliwa nna mrembo mrembo Magi huku Bale akisubiri kupewa nguvu na mrembo Emma Rhys-Jones na Robert Lewandowski akisubiri sapoti kwa kushangiliwa na mrembo Anna Lewandowska.

ZURICH, USWISI.MIAMBA 16 iliyotinga kwenye hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imeshapatikana.

Kwenye orodha hiyo kuna vigogo watupu wakiwamo Real Madrid, Barcelona, Bayern Munich, Manchester United, Manchester City, Paris Saint-Germain, Juventus, Atletico Madrid, Liverpool, Tottenham Hotspur na wababe wengine kibao, ambao masupastaa wake wataonyesha ubabe wa kibabe kwenye raundi hiyo.

Kwa maana hiyo, kutokana na idadi hiyo ya timu, kwenye hatua hiyo ya mtoano, utazamia kuwaona wakali kama Neymar, Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, David De Gea, Dele Alli, Mohamed Salah, Robert Lewandowski, Gareth Bale, Raheem Sterling, Antoine Griezmann na wengineo. Kuwapo kwa sura hizo matata, zitafanya mikikimikiki hiyo ya raundi ya mtoano kuwa na mvuto kutokana na warembo wa wanasoka hao bila ya shaka wataonekana majukwaani kwenda kuwasapoti waume zao. Unaambiwa hivi, kwenye soka, wachumba wamekuwa wakiwaongezea mzuka wanasoka ambao ni wachumba zao ili kufunga mabao ambayo mara nyingi wamekuwa wakiyatoa maarufu kwa wandani wao hao.

Hakika wachumba hao wanakwenda kuishika Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye hatua hiyo ya mtoano. Uwepo wa Ronaldo, unamfanya mrembo Georgina Rodriguez asikosekane uwanjani kumtazama habi wake, sawa na itakavyokuwa kwa staa Neymar, ambaye mrembo wake wa Kibrazili, Brona Marquezine atakuwa uwanjani kumsapoti bwana wake kama ambavyo amekuwa akifanya mara nyingi. Kipa namba moja wa Man United, David De Gea, bila shaka atamtarajia mrembo wake, Edurne Garcia kuwapo jukwaani kwenye mechi za raundi ya mtoano huko Ulaya, huku Dele Alli atakuwa kwenye kelele za kushangiliwa na bebi wake matata kabisa, Ruby Mae.

Messi kama kawaida anatarajia kuwa na sapoti kutoka kwa mrembo wake, Antonella Roccuzzo, huku Griezmann akisubiri kupata sapoti ya kutoka kwa mrembo wa nguvu, Erika Choperena na Mo Salah atakuwa na shangwe za kushangiliwa nna mrembo mrembo Magi huku Bale akisubiri kupewa nguvu na mrembo Emma Rhys-Jones na Robert Lewandowski akisubiri sapoti kwa kushangiliwa na mrembo Anna Lewandowska.

Hiyo ni orodha chache tu ya warembo wanaotazamiwa kuwasapoti waume zao katika hatua hiyo ya mtoano kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.ni muhimu kweli kweli katika kuusaka ubingwa huo wa Ulaya, ambao kwa sasa unashikiliwa na Los Blancos.