Madee afunguka ya Janjaroo, Uwoya

Muktasari:

  • Mwanamziki Madee ambaye ni Mlezi wa Dogo Janja amepiga kuwa alihusika na kumfanyia mpango Janjaro kumpata Uwoya “Daah! Hayo madai ni makali sana aisee, mimi mbona sihusiki hata kidogo,”alisema Madee.
  • Kuelekea mchezo wa Watani makundi mbalimbali ya nmashabiki wa Timu hizo hujitokeza na kuanza kuonesha ubavu wao hasa kwa kujiita majina tofauiti

WATU wamezoea kumuita baba mlezi wa Dogo Janja, lakini jina lake analotumia kwenye muziki ni Madee.

Ni msanii wa bongo fleva, makazi yake ni Manzese, Dar es Salaam. Ni mmoja na waanzilishi wa Tip Top Connection lenye maskani yake Manzese, ila kwa sasa kundi hilo limekuwa kimya muda mrefu, Madee leo anatueleza ishu nzima pamoja na maisha nje ya sanaa.

Mwanaspoti: Habari yako?

Madee: Nzuri, habari ya siku?

Mwanaspoti: Salama, hivi kundi la Tip Top ndio limekufa kabisa?

Madee: Hilo kundi limebaki jina tu, kwani kila mtu anafanya kazi kivyake. Kiufupi halipo, ila mtu akilitaka likafanye shoo watu wapo, wanakwenda kupiga mzigo fresh.

Mwanaspoti: Sasa kwanini limevunjika wakati mlikuwa mnawakilisha fresh tu?

Madee: Ni kweli tulikuwa vizuri ila ukiniambia nikueleze sababu ya msingi kweli hakuna, japo ushindani wa makundi kwa sasa kumekuwa hakuna, zamani kulikuwa na TMK, Wachuja nafaka, Hot Pot Family, Chemba Squad, Tip Top na vingine vingi. Hii ilikuwa inaleta uhai wa makundi kudumu kutokana na ushindani uliopo tofauti na sasa hakuna kitu kama hicho.

Mwanaspoti: Kumbe! watu wanasema sababu ya Babu Tale kukimbilia kwa Diamond na kulisahau kundi lake la Tip Top ndio maana limekufa.

Madee: Hakuna kitu kama hicho bwana weee, mbona kundi lilikuwa linaendelea muda mrefu bila yeye.

Mwanaspoti: Hebu tuambie maisha yako ya kila siku yakoje, ukiachana na inshu za muziki?

Madee: Aisee, maisha yangu ya kawaida sana, sina tofauti na watu wengine, tena wakati mwingine naweza sema nimewazidi sababu mmi ni mtoto wa uswahilini, hivyo nina maisha ya kiuswazi.

Mwanaspoti: Vipi maisha yako tangu umekuwa maarufu na kabla hapo, kuna tofauti gani?

Madee: Yaani tofauti ni kubwa sana, kwa sasa nimeweza kufahamiana na watu wengi, na nimeonekana kwa wengi kuwa mshauri wa mambo yao, pia shughuli zangu za kazi nazifanya kwa urahisi tu.

Mwanaspoti: Naona mtoto wako, Chonde unamuweka katika mazingira ya kiustaa, yaani mdogo lakini ni bonge la staa?

Madee: Hahahaha.... Chonde ameshakuwa staa zaidi yangu baba yake, na hii imetokana na uwezo mkubwa wa kutambua jambo kwa urahisi, anaweza kufanya kitu kama mtu mzima. Ana damu ya kupendwa ndio maana unaona watu wengi wanamfuatilia katika ukurasa wake wa Instagram, nilivyoona hivyo nikaamua kutupia baadhi ya vituko vyake.

Mwanaspoti: Enhee! vipi hali ya Dogo Janja ,anaendeleaje?

Madee: Tunamshukuru Mungu anaendelea vizuri kwa sasa.

Mwanaspoti: Ni kweli kilichomlaza hospitali ni kuachana na Irene Uwoya?

Madee: Yaani nilijua tu tunapoelekea utaniuliza swali hilo hahaha.....hiyo sio sababu, Dogo Janja na Irene hawajaachana kabisa, mie nasikia tu watu wanasena wameachana wakati hakuna kitu kama hicho

Mwanaspoti: Inasemekana wewe ndio uliyemfanyia mpango Dogo Janja kwa Irene Uwoya?

Madee: Mpango kivipi yaani?

Mwanaspoti: Inadaiwa kuwa kutokana na Dogo Janja kuweka hisia zake wazi za kumpenda Irene Uwoya kimapenzi na kusema kwenye vyombo vya habari na watu wake wa karibu kujua, wewe ulichukua jukumu la kuwakutanisha, siku hiyo Janja alikuwa na pesa kinoma, hapo ndipo walipoanza uhusiano wa kimapenzi na baadaye ndoa kabisaa.

Madee: Daah!!! Hayo madai ni makali aise, mimi mbona sihusiki maana nimejua kama mlivyojua nyie tu, basi nikaamua kuwabariki na nikaona huwezi mtu kukatisha mapenzi ya watu utaonekana mwanga hahaha......

Mwanaspoti: Asante sana kwa ushirikiano na kutupa muda kuzungumza nasi.

Madee: Nashukuru sana.